.
JIKONI FESTIVAL TANZANIA ni jukwaa la kitaifa linalotumia chakula kama kiunganishi cha uzalishaji, viwanda, masoko, uwekezaji, utalii, utamaduni, mazingira na uwezeshaji wa kiuchumi.
Tofauti na tamasha la chakula linalolenga maonesho na burudani pekee, JIKONI imeundwa kuwa jukwaa la soko na ukuaji wa biashara, likichanganya maonesho na mauzo, usindikaji na viwanda vidogo, pamoja na kuwezesha mahusiano ya B2B.
Dira: Kuwa jukwaa kuu la Kitaifa linalounganisha chakula, biashara, uwekezaji, utamaduni na maendeleo ya jamii.
Lengo Kuu: Kukuza mnyororo wa thamani wa chakula na vinywaji Tanzania kupitia ukuaji wa masoko, Viwanda, uwekezaji, uwezeshaji wa wajasiriamali na Utalii wa Chakula.
Maonyesho & Biashara
Wahusika: Mama Lishe na Baba Lishe.
Pilau, biryani, wali, ugali, ndizi, chipsi, vitafunwa, street food na vyakula vya asili.
Wahusika: Wachoma Nyama / Wamiliki wa Majiko.
Nyama choma, BBQ, kuku, mbuzi, ng'ombe, samaki, dagaa, kamba na vyakula vya baharini.
Wahusika: Kampuni, viwanda na wadau.
Kahawa, chai, cocoa/chocolate beverages, juices za asili na vinywaji vya mimea.
Wahusika: Wakulima wa zabibu, Viwanda na Wauzaji.
Wachakataji, Viwanda vya Mvinyo, Chapa za mvinyo na wadau wa mnyororo wa thamani.
Wahusika: Wakulima, Wauzaji na Wasambazaji.
Viungo, asali, bidhaa za nyuki, herbs, sauces, seasonings na natural food products.
Wahusika: Wakulima na Wasambazaji.
Organic foods, matunda, mboga, nafaka, pulses, lishe, healthy snacks na fortified foods.
Wahusika: Viwanda vya uchakataji na Teknolojia.
Mashine za kusaga/kukausha/kufungasha, mifumo ya kugandisha, vifungashio, vifaa vya kupikia na Nishati Safi.
Jikoni Festival inatekelezwa kwa ushirikiano wa karibu na Wizara za Kisekta ili kuimarisha mnyororo wa thamani:
Muongozo wa nishati safi ya kupikia, uchumi mzunguko, na fursa za uchumi wa kijani.
Kuratibu utekelezaji katika ngazi ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Uboreshaji wa bidhaa, kuendeleza viwanda vidogo, na kuunganisha na masoko/mitaji.
Kuthibiti usalama wa chakula, kuongeza thamani ya mazao na kuunganisha na masoko.
Kukuza uzalishaji, usindikaji na fursa za uwekezaji kwenye sekta ya mifugo na uvuvi.
Kukuza utalii wa chakula, vyakula vya asili, ufugaji nyuki na matumizi ya maliasili.
Kuvutia wawekezaji wa kimataifa na kutumia festival kama diplomasia ya uchumi.
Uwezeshaji wa Mama Lishe, wanawake, na makundi maalum kiuchumi.